In the Name of Allah, The Most Gracious, Ever Merciful.

Love for All, Hatred for None.

Browse Al Islam

 

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWINGI WA UKARIMU

JUMUIYA YA WASILAMU WAAHMADIYYA KATIKA ISLAM


Kadri siku zinavyopita, watu zaidi wanauliza: Jamani, hii Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya ni kItu gani? Mbona inayazagaa makontinenti mazima mazima upesi upesi? Ni akina nani hawa wanaomzungumzia Mwenyezi Mungu, na Islam na kudai kuwa Waislamu halisi, na kumbe wanakataliwa na Waislamu wengine? Wanazungumzia upendano, amani, na kuwahudumia wanadamu. Kulikoni basi? Ni nani mwenye kuendesha na kusimamamia Jumuiyya hii? Bali na hela je? Maswali haya yote na mengineyo mengi yanaulizwa, mengine kwa nia njema ya kutaka kujua, ilihali mengine ni kutokana na kijicho na hata husuda. Kwa kuwa uvumi chungu nzima unaenezwa, sisi tutajaribu kutoa kimuhutasarl majibu baadhi ya maswali haya. Nduguwanaotaka kujua habari zaidi wanatafadhalishwa wawasiliane nasi kupitia annuani iliyoandikwa mwishoni mwa makala haya.

Mwanzo kabisa , ni kumhusu mwenyezi Mungu. Naam, sisi twazungumzia mwenyezi Mungu, twamzungumzia Allah. kwa kuwa yeye ndiye Mwanzo na Mwisho wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya, au kwa ufupi, Ahmadiyya pia ni kwa sabau Mungu, wetu ni yule Mungu aliye hai, Mungu wa Mtume mtukufu Muhammad, s.a.w., Mungu wa Manabii wote na Mungu wa masihi na Mahdi aliyeahidiwa - ambaye ndiye Nabii wa zama hizi za mwisho na mwanzilishi wa Jumuiya hii, Basi Mungu wetu ndiye Mungu wa Kurani Tukfu. Twamwamini Yeye, manabli wake, malaika na siku ya hukumu.

"Sema, yeye ni Allah, Mmoja Allah, asiyehitaji, wote wanahitaj kwake. Hazai wala hakuzaliwa, na hapana afanana naye". (Kuranitukufu,.Sura Al-Ikhlas, aya ya 2 - 5).

Sisi twaapa na kushuhudia kwamba Yeye kwa hakika ni Mungu aliye hai, azungumzaye na Manabii na watakatifu na apendapo, hata huzungumza na wenye dhambi. Alizungumza hapo zamani na yuwazungumza hata hivl sasa. Yeye hakuumba mwanadamu kumtupilia mbali ulimwengunl (universe) ajiruzuku yeye mwenyewe na kujaribu kujitafutia mahali pake. Aiipeleka manabii kwa mataifa yote kuwaongoza wanadamu kwenye njia iliyonyooka. Sisi twawaamini manabii wote kama sehemu ya imani yetu, kila mmoja wao alitumwa kwa watu mahususi kwa. muda mahususi. Lakini mwanadamu alikuwa sasa amefikia ukamilifu wake, Ulikuwa ni wakati wa ujaji mkuu, ujaji wa mtume mtukufu Muhammad s.a.w.

"Sema, enyi watu, hakika mimi ni mtume kwenu nyote atokaye kwa Allah ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi," (Kurani Tukufu, Sura Al-A’ 159)

Akiwa Nabii kwa ulimwengu mzima. sisi tu kwamba Islam ilipunguza wingi wa miungu hadi Mungu mmoja na utengano hadi utangamano, bali cha zaidi, kwa ujaji wa Mtume Mtukufu (saw) dini iliyofunuliwa ilikuja.kuwa utaratibu mmoja wa kimabadiliko wenye maana, uliofikia kilele chake kwenye dhati tukufu ya Mtume Mtukufu Muhammad (saw), Kwa fadhila za mwenyezi Mungu na katika kutimiliza bishara iliiyofanywa Bwana wake mtakatifu na mwongozl wake, - mtume mtukufu Muhammad s.a.w, mwanzilishi wa jumuiya ya waislamu Waahmadiyya aliirejesha tu ile Islam ya mtume mtukufu katika usafi wake wa asili. Huyu mwanzilishi mtakatifu wa jumuiya ya waislamu Waahmadiya yuwasema:

"Enyi mnaoishi Juu ya uso wa ardhi, na nyoyo zote za wanadamu zilizoko mashariki au magharibi, nawatangazieni kwa dhati kwamba ukweli halisi ni Islam peke yake na Mungu halisi ni yule Mungu anayeelezewa katika Kurani na Nabii mwenye uzima wa milele wa kiroho na anayekalia kiti cha enzi cha taadhima na utakatifu ni Muhammad, mteule. s.a.w. Dalili uzima wake wa kiroho na taadhima takatifu ni kwamba kwa kumfwata na kumpenda sisi, tunakuwa wapokeaji baraka takatifu ya kuzugumza na mwenyezi Mungu na tunashuhudia ishara za kimbinguni (Tiryaq-ul-Quloob, Ruhani, Khazain,Jal15,uk.141).

Ujaji wa Mtume mtukufu s.a.w. ulikuwa bado ndilo tukio kubwa zaidi lililopata kutukia au litakalopata kutukia historiani. Dini zote zikaunganika kufanya dini moja ya kiulimwengu mzima kwa amri ya Mungu. Kurani tukufu zaidi ya hazina yake kuu ya ukweli wa azali, pia ikajikusanyia ule ukweli uliokuwemo ndanl ya vitabu vya hapo awali na Ikafadhahisa kuwaamini manabii wote. Kurani Tukufu ilikuwa bado hata hivi sasa ni mwongozo wa wakati wote na wa watu wote. Mikononi mwa Mwekaji mtakatifu wa mfano bora s.a.w, ulimwengu tayari umeishaona ule muujiza wa mapinduzi makubwa zaidi ya kitabia uliowageuza watu waliokuwa wanyama wa mwituni na kuwafanya watu watakatifu.

Hata hivyo, Mtume Mtukufu s.a.w, alitabin kwa masikitiko makubwa ya kwamba katika zama za mwisho wafuasi wake wataipotea njia iliyonyooka na kuporomoka kwenye hali za chini zaidi za udhalifu wakati huo, Mwenyezi Mungu katika huruma zake zisizokua na mwisho Atamfanya yute masihi na mahdi aliyeahidfwa adhihiri kuwaokoa wanadamu na kuwarudisha kwa Mungu na Islam.

Bali ukweli wehyiewe ni kwamba wafuasi wa dini zote kubwa kama vile Mayahudi, Wakristo, Mabaniani, na wangineo, nao pia walikingojea, kwa hamu na dhamu ujaji wa huyo mdhaminishaji (Re-former) Aliyeahidiwa sawa na vile ilivyotabihwa katika vitabu vya dini. Ama kusema kweli. hali zenyewe (za kidunia) za kustahilishia ujaji wa huyo mdhaminishaji aliyeahidiwa zilikuwa zimetayarika kabisa.

Enyi rafiki zetu jueni ya kwamba kama vile ilivyotabiriwa, ujaji huu wa mdhaminishaji wa dini zot.e aliyeahidiwa tayari umeshafanyika katika dhati ya hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (1835 - 1908) wa huko Qadian, kijiji kimoja nchini India. Kwa amri ya Mungu, na katika kutekeleza ile bishara juu ya ujaji wa mdhaminishaji aliyeahidiwa, yeye hapo mwaka wa 1889 alisimika msingi wa ile ambayo hivi leo ni hii Jumuiya iliyo mbioni katika Islam, ya Ahmadiyat. Akiwa mwana wa kiroho na mfuasi wa mtume mtukufu s.a.w. yeye alitumwa na mwenyezi Mungu aje airudishe tena Islam kwenye usafi wake wa asili na kwa sababu hiyo kuziunganisha na kuziwakilisha dini zote iliofunuliwa. Yeye pia alitangaza kuwa ndiye masihi na mahdi aliyeahidiwa, na kwamba yule masiha mwana wa Maryamu kamwe hatarejea, kwani baada ya kuokolewa kutoka msalabani, alifariki kifo cha kawaida na kwamba roho yake ilikuwa ikipumzika kwa amani huko mbinguni. Hali kadhalika yeye alitangaza kwamba Mungu bado yuwazungumza na kwamba yeye mwenyewe alikuwa ni mpokeaji wa maneno ya Mwenyezi Mungu na akatamka akisema:

"Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, aliye mdhamini wa uhai wangu ya kwamba ni Yeye ambaye amenituma. akaniita nabii, na akaniita masihi aliyeahidiwa. Yeye ameonyesha ishara kubwa kubwa za kuungia mkono madai yangu, ambazo ni tekriban 300,000.

(Nyongeza ya Haqiqa-tul-Wahi, Ruhani Khazaini, Ja. 222, uk. 503)

Kama, ilivyotarajiwa, tangazo lake kama yeye ndiye aliyekuwa ni masihi na mahdi aliyeahidiwa, tena nabii wa zama hizi za mwisho, lilijibiwa kwa makelele ya chuki na ukataaji wa katakata. Waislamu, Wakristo, na viongozi wa kidini wakaungana pamoja kukikomesha mara moja kile walichokidhanj kuwa ni upotovu dhahiri, Bali upinzani dhidi ya Jumuiya hii bado waendelea bila ya kuzuzi. Hata serekali na mashirika (ya kidunia) kwa kuongozea yakajiingiza kwenye upinzani au tuseme kwenye vita dhidi ya Jumuiya. Kwa muda wa miaka mia moja iliyopita, kila juhudi zimefanywa kuivunjilia mbali Jumuiya hii. Waahmadiyya walipigwa mawe hadi wakafa - kama vile ule Afghanistan, walipigwa visu hadharani, waliuawa, nyumba zao zikaporwa na kuteketzwa mbali. Walinyimwa haki zao za kimsingi za kuamini, kudhihirisha na kufuata imani yao - kama vile huko Pakistan. Waahmadiyya walitangazwa kiserikali kuwa sio Waislamu, hawakuruhusiwa mahali wanapomwabudia Mola wa walimwengu kupata ‘Msikiti’ au kuadhini, bali hata kuamkia (assalaamu alaikum) kama waislamu. Harakati za chuki na ukomeshaji na husuda zikaanzishwa kwa msaada na idhini ya kiserikali, kiasi hiki kwamba hata kiongozi mkuu wa jumuiya akaona haiwezekani kutekeleza wajibu wa.madaraka yake ya kiroho na ikabidi aitoke Paklstan.

Tangu kuanzishwa kwake, licha ya uhasama wenye kuongezeka na zile mbinu potovu ambamo upinzani wa kila aina unahamakishwa, Jumuiya hii imeendelea kujichumia watu walio mashujaa kiasi cha wao kuwa tayari kulipia thamani ya ukweli. Wakati mwanzilishi mtakatifu aliporudishwa kwa muumba wake hapo mwaka wa 1908, watu walifikiria kwamba Jumuia itafifia na kujifilia mbali. Lakini siku baada ya siku, iliendelea kustawi chini ya uongozi uliochaguliwa na kuteuliwa kimbinguni wa makhalifa watatu wa kwanza wa mwanzilishi mtakatifu. Mtukufu khalifa wa sasa wa nne kuchaguliwa, kama vile watangulizi wake naye pia ni mteule wa Mwenyezi Mungu na ndiye mbiu ya mgambo wa zama hlzi. Kwa fadhili za Mwenyezi Mungu, chini ya Uongozi wake wenye kutia shime, Jumuiya hil imeambulia kupiga hatua kubwa. Milango ya rehema za kibinguni ni kana kwamba imefunguliwa kubwa. Milango ya rehema za kimbinguni ni kana kwamba imefunguliwa wazi kabisa. Watu toka duniani kote wanakusanyika kujiunga na jumuiya kwa idadi inayozidi kuongezeka daima kama inayvoonyesha orodha iliyo hapo chini. Mwaka jana tu, kwa mfano, wanajumuia wapya milioni kumi na moja walijiunga na jumuiya, mwaka huu Idadi ya watu wapya waliojlunga ilikuwa zaidi ya milioni arobaini.

Jumuiya za waislamu waahmadiyya hivi sasa zapatikana katika nchi 170 duniani. Televisheni ya kiahmadiyya (Muslim Television Ahmadiyya (MTA) ya tapanya mafundisho ya kiislamu kwa dunia nzima, masaa 24 kila siku. Jumuiya hii imefikisha maandiko ya ujumbe wa Kurani Tukufu kwa wanadamu walio wengi zaidi kwa njia ya kueneza tafsiri za kitabu hiki kitakatifu katika lugha kubwa 53 za dunia. Jumuiya imetilia maanani maendeleo ya huduma za kijamii za baadhi ya wanadamu walio nyuma kimaendeleo kwa kuanzisha miradi kabambe ya kielimu na kiafya katika nchi kadha za Kiafrika. Tunakualikeni mkajihakikishie nyinyi wenyewe ukweli juu ya. Jumuiya hii. Mkitataa kuitikia mwito wa kimbinguni na kujiunga na jumuiya, sisi tutawakaribisheni kama ndugu na dada zetu mliotupotea jumuiya, sisi tutawakaribisheni kama ndugu na dada zetu mliotupotoa kwa muda mrefu. Lakini kumbukeni, kujiunga na jumuiya ni jambo (inalohitaji imani safi, kuwajibika, na kujitolea. Sio kama kujiunga na klabu au msafara wa kitalii. Nasi wala hatuna lilio bora la kuwaambieni zaidi ya kumkariri masihi na mahdi mwenyewe aliyeahiiwa.

"Msitosheke na kule kufanya ahadi ya Bai’at, kwani hiyo si chochote. Mwenyezi Mungu hutazama nyoyo zenu naye atawatendeeni sawa na vile zilivyo."

(Saflnaya Nuhu, Ruhani Khazairn, Jal. 19, uk.18)

Kiini cha Islam kinayo mambo mawili. Kwanza, ni kwamba Mwenyezi Mungu Mweza awe ndiye shabaha ya ibada na lengo halisi na mpendwa halisi, na kwamba mwenginewe yeyote asishirikishwe katika ibada Yake. Katika mapena yake na katika matumaini juu yake. Jambo la pili la mtu kujitolea maisha yake katika njia ya Mwenyezi Mungu Mweza ni kwamba maisha ya mtu yawe yatewekwa wakfu kwa ajili ya kuwahudumia viumbe Vyake na kuwahurumia na kwa ajili ya kuwa pamoja nao katika shida zao na huzuni zao.

(ayeena-e-kamalat - e – Islama, Ruhani Khazaini, Jal. 5, uk. 60)

"Kama mkiwa wa Mwenyezi Mungu, basi kuweni na hakika kwamba Mwenyezi Mungu ni wenu. Mtakuwa mmelala na Mwenyezi Mungu atawakalieni macho. Mtakuwa vazembe juu ya adui wa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu atamchunga na kupotosha hila zake. Mwenyezi Mungu ni hazina yenye thamani basi mthamini vile inavyowalazimu. Kwani Yeye ndiye Msaidizi wenu katika kila hatua.

(Safina ya Nuhu, Ruhani Khazain, Jal. 19, uk.22).

Hatimaye, tungeliipenda kuwashauri kutoujali udanganyifu na uwongo uenezwao ne viongozi wa dini na watu wengine, fikeni shinani nyingi wenyewe kutafuta ukweli. Kumbukeni, sisi tu jumuiya iliyo peupe wala si Jumuiya ya kisirisiri katika maana yoyote ya neno hili.Wanajumuiya wetu. wanaume, wanawake, na watoto wanavyo vitengo vyao katika jumuiya sawa na makamo ya umri wao, wote wakiwa ni matawi ya vitengo vyao vya kitaifa na vya kimataifa. Hali kadhalika, kila mwanajumuiya huchanga sehemu ya kipato chake kwenye mfuko wa Jumuiya ili kusadia katika kugharamia mtandao mpana sana wa Jumuiya hii katika gazi ya shinani, kitaifa na ngazi ya kimataifa duniani kote, zikiwemo misheni zetu, taasisi za elimu, mahospitali, viwanda vya uchapishaji na uenezaji, vitabu, mijala na magazeti, mikutano yetu, n.k. Hesabu za pesa za jumuiya zinakaguliwa vilivyo na bajeti za mapato na matumizi kupitishwa kwenye ngazi ya shinani, kitaifa na ngazi ya kimataifa. Mnaweza mkachanga kwa hali na mali mbali na hata wakati. Mnaweza mkajitolea maisha yenu mazima au sehemu yake.. Mnaweza pia kuwatoa wakfu watoto wenu kwa ajili ya Kumtumikia Mwenyezj Mungu na viumbe Vyake, kwa sharti la kuthibitisha ahadi au kuitangua zama mtoto anapokuwa mtu mzima. Lakini kumbukeni, cha msingi katika kila kitu, ni huu ukweli ya kwamba sharti, kadhiri tunavyokuwa na ufasiri na bahati njema ya kudumu tukiwa wanajumuiya, tusiamini tu bali tutende pia na kiishi maisha ya ukweli - yaani, Islam. Mwatakiwa kusali sala tano za kila siku, kusoma Kurani Tukufu kila siku, na kumsalia Mtume Mtukufu (s.a.w).

"Mwenyezi Mungu ni tajiri Mkubwa. Ili kumpata hamna budi kuwa tayari kukumbana na taabu. Dumisheni sala, dumisheni sala kwani kwani sala ndio ufunguo wa bahati zote njema. Kuweni wakweli, kuweni wakweli kwani Mwenyezi Mungu yuwazitazama nyoyo zetu. Je mwanadamu anaweza akamdanganya?" (Izala-e-Auha, Ruhani Khazain. Jal. 3. uk. 549)

.Lililo la mwisho lakini silo dogo, twawakumbusha wanajumuiya wote - wapya na wa zamani ya kuwa katika kuonyesha shukrani kwake Mwenyezi Mungu, natujeni uhusiano wenye kudumu wa kumheshimu kwa dhati khalifa wetu mtukufu wa hivi sasa - Mwenyezi Mungu na amlinde na kumpa maisha marefu. Na tuwasiliane naye, kumwombea na kujichumie dua zake ambazo kwa hakika ni zenu pia hata bila nyinyi kutaka kuombewa.

MWAKA

IDADI YA WANAJUMUIYA WAPYA

1994 - 1995

845,294

1995 – 1996

1,602,721

1996-1997

3,004,584

1997 - 1998

5,004,591

1998 - 1999

10,820,226

1999 – 2000

41,308,975

 

Kimeenezwa na

E.A. AHMADIYYA MUSLIM MISSION

S.L.P. • Simu: 254-2-764226

NAIROBI — KENYA

 

AHMADIYYA MOVEMENT IN ISLAM AN INRODUCTION

(Swahili Language)