In the Name of Allah, The Most Gracious, Ever Merciful.

Love for All, Hatred for None.

Browse Al Islam

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWINGI WA UKARIMU

 

MASIHI NA IMAM MAHDI AMEKWISHA FIKA TAYARI


BISHARA kuhusu ujaji wa Kiongozi mkubwa kiroho hupatikana katika dini zote takriban. Na huu ndio wakati ambapo wafuasi wa dini zote wanamngoja huyo Kiongozi kwa hamu na kiherehere.

Kwa kuwa bishara hizo zimeiajwa kwa uwazi zaidi katika vitabu vya Kiislamu na vya Kikristo, hivyo twapenda kueleza habari hii kulingana na dini hizo mbili.

Waislamu kwa Wakristo wanaamini kwamba Nabii Isa (a.s.) au Yesu Kristo atashuka kutoka mbinguni. Jambo la muhimu kuhusu habari hii ni kwamba Nabii Isa (a.s.) hakufa msalabani wala hakupaa mbinguni, bali alikufa kifo cha kawaida. Na anayekufa harudi duniani tena. Hivyo, swali la kurudi Nabii Isa (a.s.) wa zamani haliwezi kuzuka.

Muradi wa bishara kuhusu kuja kwa Nabii Isa (a.s.) mara ya tena, ni kwamba mwingine aiakayefanana naye atakuja na kwa njia hii bishara itaiimia.

Hakika yenyewe ni kwamba kufika mara ya pili kwa Mtume wa zamani katika lugha ya kidini kunamaanisha kwamba mtu mwingine atakayefanana naye kiroho atafika. Nabii Isa (a.s.) ambaye bishara ya kuja kwa Masihi aliyeahidiwa inamhusu yeye moja kwa moja, mwenyewe atifafanua jambo hili kwa uwazi sana.

Nabbii Isa (a.s.) alipodai kuwa yu Masihi, Mayahudi walipinga wakisema, Eliya aliyepanda mbinguni (2-Wafalme 2:11) ateremke kwanza kutoka mbinguni. Lakini Nabii Isa (a.s.) aliwafahimisha kwamba habari ile ilikuwa ni mithali tu na hakika yake ni kwamba angefika mtu mwingine akifanana na Eliya.

Kasema Nabii Isa (a.s.): "Kweli Eliya atakuja ayaweke mambo yote katika mpango, lakini nawaambieni, Eliya amekwisha kuja nao hawakumtambua, bali walimtendea jinsi walivyotaka. Mwana wa Adamu atateswa vivyo hivyo mikononi mwao. Hapo hao wanafunzi wakafahamu kwamba alikuwa akiwaambia juu ya Yohana Mbatizaji (Mathayo 17:11-13).

Nabii Isa (a.s.) kwa kuwatolea wafuasi wake mfano huu, aliwafahamisha kwamba kama vile bishara ya kufika Eliya ilivyotimia katika dhati ya Yohana Mbatizaji, hivyo ndivyo itakavyokuwa kujt) kwake mara ya pili. Yaani si yeye mwenyewe atakayekuja. bali mfano wake yeye atafika,

Si hayo tu, bali Mtume Mtukufu Muhammad S.A.W, aliyetabiri ufikaji wa Masihi, alisema kwa uwazi sana kwamba Masihi atatokea katika Waisiamu. Alivyosema Mtume S.A.W, ni kwamba, "Mtakuwaje aiakapofika Mwana wa Mariamu kati yenu, naye atakuwa Imam wenu kutoka miongoni mwenu..." (Bukhari). Maneno "KUTOKA MIONGONI MWENU" yanahakikisha wazi kabisa kwamba Masihi aliyeahidiwa, atatokana na Waislamu ambaye; atazaliwa katika Waislamu.

Tungependa kuwapasha wanadamu wote habari njema kwamba yule Kiongozi aliyetazamiwa kufika, aliyekuwa akingojewa kwa hamu na kiherehere na mataifa yote, amekwisha fika tayari, naye ndiye Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad wa Qadian, India (1835-1908),

HADHRAT MIRZA GHULAM AHMAD (A.S.)

Mwanzilishi Mtakatifu wa Jumuiya ya Waislamu Waahamadiyya, Ametumwa na Mwenyezi Mungu ili kuwaongoza watu wote kwenye dini ya kweli nayo ndiyo ISLAM. Ni mwana wa kiroho wa Mtume Mtukufu Muhammad S.A.W. aliyepata cheo cha Unabii katika utii na ufuasi kamili wa Bwana wake Muhammad S.A.W.

Twataka kusema maehache juu ya ukweli wa Mwanzllishi Mtakatifu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya. Kurani Tukufu yatuambia kwamba Mitume wa Mungu daima hushinda (58:22), Na vile vile, Intuhakikishia kwamba mwenye kumzuilia Mungu uwongo sio tu kwamba ananyimwya msaada wa Mungu, bali hupata adhabu kutoka kwa Mungu (69:45-48). Kununi hii ya mwongo kuadhiniwa imetajwa katika Biblia pia (Kumbukumbu 18:20; 13:5).

Ijapokuwa Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (a.s.) alikabili upinzani mkali kutoka kwa Waislamu, Wakristo na wafuasi wa dini nyingine, lakini ni yeye aliyepata ushindi na kufaulu kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na leo hii sauti yake inasikika katika dunia nzima na Jumuiya Ahmadiyya kwa fadhili za Mwenyezi Mungu imesitawi katika nchi zaidi ya 130. Kinyume chake,wapinzani wake walishindwa na kufedheheka nao wanaendelea kufedheheka hadi leo. Wako wapi akina Bhutto na Zaia-ul-Haq wa Pakistan na Idi Amin wa Uganda?

Mtukufu Mtume Muhammad S.A.W. vile vile alitabiri kutokea ishara mbili za maana sana wakati atakapokuja Masihi na Imam Mahdi. Mtume S.A.W. alisema: "Hakika kwa ajili ya Mahdi wetu kuna ishara mbili ambazo hazijapata kutokea tangu kuumbwa mbingu na ardhi, nazo ni: "Mwezi utapatwa usiku wa kwanza katika Ramadhani, na Jua litapatwa katikati katika mwezi huo" (Dar Qutni, J.I. Uk.188). Tena, ishara hizi zimetajwa hata katika vitabu vya zamani zikiwa ishara za kufika Yesu mara ya pili, kama yeye Yesu mwenyewe alivyosema: "Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake" (Mathayo 24:29).

Ishara hizo za kimbinguni zilitimia mnamo mwaka 1894(1311 A.H.) ambapo katika Ramadhani mwezi ulipatwa ya kwanza katika tarehe za kupatwa kwake yaani 13 na Jua likapatwa terehe ya katikati yaani tarehe 28.

Mwanzilishi Mtakatifu wa Jumuiya Ahamadiyya alopodai kuwa ametumwa na Mwenyezi Mungu na kwamba yu Imam Mahdi, Masheik wa India walimpinga vikali wakisema, "Mbona zile alama za kupatwa Jua na Mwezi katika Ramadham zilizotajwa kaiika Hadithi ya Mtume S.A.W. hazikutimia?" Lakini ajabu ni kwamba atama hizo zilipotimia, Masheikh wale wale walianza kupiga kelele wakisema, "sasa watu watapotea". Walikuwa na maana kwamba ishara za ukweli wa Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (a.s.) zimetimia tayari, hivyo watu watamwamini na kujiunga na Jumuiya yake.

Kwa neno zima, bishara ya kuhusu ujaji wa Masihi na Imam Mahdi imekwisha timia tayari katika dhati tukufu ya Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (a.s.). Mwenye masikio na asikie. Kama si yeye, ni nani aliyetokea badala yake? Au, je, mtaendelea kumngoja yule Masihi Mnazareti kama vile Mayahudi wanavyoendelea mpaka leo kumngoja Eliya ashuke kutoka mbinguni, lakini yeye haji wala hatakuja kamwe. Hivyo ndivyo mtakavyoendetea kumngoja Nabii Isa (a.s.) mwenyewe atokee mpaka mtachoka, lakini yeye hatakuja katu.

Mwanzilishi Mtakatifu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya, Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (a.s.) akitabiri, alisema mnamo mwaka 1903: "Kumbukeni, hakuna atakayeshuka kutoka mbinguni. Wapinzani wetu wote walio hai wakati huu, watakufa wala hakuna hata mmoja kati yao atakayeshuhudia Isa bin Mariam kuteremka kutoka mbinguni. Kisha kizazi chao kitakachobaki nacho kitakufa wala hakuna yeyote atakayeona Isa bin Mariam kushuka kutoka mbinguni. Bali kizazi cha kizazi hicho nacho kitakufa bila kushuhudia mwanaye Mariam kushuka kutoka mbinguni. Hapo Mungu Atawatilia wasiwasi na mahangaiko nyoyoni mwao kwamba zama za ushindi wa msalaba zimekwisha pita na dunia imeingia katika hali tofauti, lakini mtoto wa Mariam hajashuka bado kuioka mbinguni. Hapo mara moja wenye busara wataachana na imani hiyo".

 

Kimeenezwa na

E.A. AHMADIYYA MUSLIM MISSION

S.L.P. • Simu: 254-2-764226

NAIROBI — KENYA

 

THE PROMISED MESSIAH AND MAHDI HAS COME

(Swahili Language)