In the Name of Allah, The Most Gracious, Ever Merciful.

Love for All, Hatred for None.

Browse Al Islam

 

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWINGI WA UKARIMU

 

YESU KRISTO HAKUTUMWA KWA WATU WOTE


Yesu Kristo anasema; "Msidhani ya kuwa nilikuja kuitangua Torati au Manabii, la, sikuja kutangua, bali kuitimiliza. Kwa maana nawaambieni, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka yodi moja na nukta moja ya Torati haitaondoka mpaka yote yatimie (Mathayo 5:18-18)"

Ni dhahiri kuwa Nabii Musa na manabii wengine watiotangulia walkuja kuwafundisha na kuwaongoza Waisraeli tu. Yesu Kristo amekwisha kubali katika maneno ya juu ya kuwa amekuja kulitimiza kusudi lile ile ya Musa na Manabii wengine waliotangulia.

Lakini tunaona mapadri wamekwisha fika katika kila sehemu ya dunia hata Afrika ijapokuwa Yesu Kristo mwenyewe hakuwa na nia na kusudi ya namna hii kabisa. Sasa swali hasa linalotakiwa kufikiriwa, si Wakristo wanafanya nini, bali ni, "Je, Yesu Kristo alikuwa na nia na azimio gani?" Mwenyezi Mungu alikuwa na kusudi gani alipomtuma Yesu Kristo? Jambo hili haliwezekani kuelezwa kwa njia nzuri na yeyote isipokuwa lielezwe na Yesu Kristo mwenyewe. Na Yesu amekwisha sema wazi "Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya lsraeli (Matt. 15:24). Tena akasema, "Mwana wa Adamu alikuja kukiokoka kilichopotea (Matt. 18:11)."

Kwa hiyo mafundisho ya Yesu Kristo ni kwa ajili ya Waisraeli tu si kwa watu wengine kabisa. Inasemekana kwanba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine kabisa, Inasemekana kwamba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine pia. "Basi endeni kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la baba na-roho mtakatifu. (Matt. 28:19)"

Lakini kushika dalili katika maneno haya kuwa Yesu Kristo aliwaamuru wafuasi wake kupeleka ujumbe wake kwa watu wengine wote wasio Waisraeli, pia si sawa. Maana Yesu Kristo amesema wazi kabisa:

"Mimi nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata katika zamani za kuzaliwa upya atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara. Mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli (Matt. 28:19). ‘Tena, "Sikupelekwa ila kwa kondoo zilizopotea za nyumba ya Israeli (Matt. l5:24). "Tena, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa (Matt. 15:26) "Sio haya tu bali pia tunasoma, "Hawa thenashara Yesu aliwatuma akawaagiza, akinena, katika njia ya mataifa msiende wala miji mwa Wasamaria msiingie; Afadhali shikeni njia kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Matt. 105-6)""

Kutoka kwa mafungu ya maneno haya ni kuwa wafuasi wake wameamrishwa naye kupeleka ujumbe wake kwa mataifa yote ya Israeli si mataifa yote ya ulimwenguni. Mtu asidhani ya kwamba mawazo ya maneno yajuuni kuwa waende kwanza miji ya Waisraeli na baadaye kwenye miji mingine. La, maana kwenda kwa kondoo waliopotea wa Israeli si maana yake kuvitazama vijiji tu, bali ni kuwaingiza katika dini ya Ukristo. Basi kwa hakika maana hasa ya maneno haya ni kuwa Waisraeli wote waingie katika Ukristo, Mkristo na padri ye yote asijielekeze kabisa kwenye mataifa mengine. Yesu Kristo amehakikisha wazi wazi ya kuwa kazi ya kuwahubiria dini Waisraeli na kuwaingiza katika njia yake haitamalizika mpaka kufika kwake mara ya pili, kama ilivyosema:

"Watakapowaudhi katika mji huu, kimbilieni mwingine kwa maana ni kweli nawaambieni, Hamtaimaliza mji yote ya Israeli hata ajapo mwana wa Adamu (Matt.10:23). "Katika maneno haya inajulikana wazi ya kuwa yaliyosemwa katika Mathayo (28:19) makusudio yake ni kwamba wahubiri Wakristo wasimamishe Ukristo katika miji ya Israeli na waingize kabila la Israeli katika dini yao si kuvitembelea tu na kuvitazama vijiji vya Waisraeli. Na pia ni wazi ya kuwa kazi hii ya kuhubiri na kuwaingizia haitamalizika mpaka Yesu Kristo aje mara ya pili. Kwa hiyo kuwahubiri watu wengine wasio katika mataifa ya Israeli ni kinyume kabisa na mafundisho na maagizo ya Yesu Kristo. Hata mitume wa Yesu pia walifahamu kuwa ni kosa kuwahubiri watu wengine wasio Waisraeli. Tunasoma:

Mimi nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata katika zamani za kuzaliwa upya atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu.

"Basi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile shida iliyotokea kwa habari ya Stefano wakasafiri hata Foiniki na Kupro na Antiokia. Wasilihubiri lile neno ila kwa Wayahudi peke yao!! (matendo11:19)." Hivyo, mitume wa Yesu waliposikia ya kuwa Petro aliwahubiri watu wasio Israeli pahali fulani, wakakasirikia nawakashindana naye:

"Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemi, wale walio wa Tohara wakishindana naye, wakisema, uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao" (Matendo 11:2-3)",

Kwa neno zima kabla ya Mtume wetu Muhammad (saw) hakuna nabii au mtume ye yote aliyeamrishwa na Mwenyezi Mungu kuwahubiri watu wote wa ulimwengu mafundisho yake. Wao walikuwa wanatumwa kwa makabila maalumu na miji kadha wa kadha. Wala hakuna dalili yoyote ihakikishayo ya kuwa Yesu Kristo alitumwa kwa makabila yote ya dunia nzima wala hakuna ishara idhihirishayo ya kuwa Yesu Kristo aliwaamuru wanafunzi wake kuwahubiri watu wa ulimwengu mzima isipokuwa alisema:

"Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Matt.15:24)," Mapadri wanaofanya kazi ya kuhubiri dini ya Ukristo katika Waafrika na watu wengine wasio Israeli kwa hakika wanafanya kinyume cha maagizo ya Yesu Kristo ? Naam, Mtume Muhammad (saw) kwa amri ya Mwenyezi Mungu alisema: "Enyi watu wote! Kwa hakika mimi ni Miumbe wa haki niliyetumwa na Mwenyezi Mungu kwenu nyote" (Kurani 7:159).

TAFSIRI ZA INJILI ZINAPINZANA

Tafsiri ya zamani ya 1 Wakorinto 7:1 ilisema:

"Basi, kwa mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asiguse mwanamke."

Na tafsiri mpya ya sehemu hiyo inasomeka hivi:

"Na sasa nataka kuwajibuni juu ya mambo mliyoandika. Mliniuliza kama ni jambo, nzuri mwanamume asikae na mwanamke."

Tafsiri ya kwanza ina maneno machache. Tafsiri mpya ina maneno

mengi. Kwa nini?

Na kwa nini.maelezo ya zamani na ya sasa yamepewa sura ya ulizo? Nenohili: MLINlULlZA limetoka wapi? Wala halimo katika tafsiri yo yote iliyopata kutangazwa hadi leo?

Hata tafsiri mpya inayoitwa HABARI NJEMA KWA WATU WOTE haina habari ya MLINIULIZA. Je, mnaharibu maksudi maneno mnayotuambia ni matakatifu?

Wala hamna faida katika kugeuza tafsiri ya kifungu cha kwanza. Kwa sababu vifungu vinne vinavyofuata vinasema nia ile ile ya ubora wa kukaa bila kuoa. Hebu someni chini yake kifungu cha 7,17, k27, 32, 34, 35, 37 na 40. Mpaka mwisho wa mlango huu wa saba, Mt. Paul anangang’ania jambo hili hili la kukaa bila kuoa kuwa bora kuliko kuoa. Sasa mtageuza mlango huu wote ili muwe na mafundisho ya namna nyingine?

Kimeenezwa na

E.A. AHMADIYYA MUSLIM MISSION

S.L.P. • Simu: 254-2-764226

NAIROBI — KENYA

JESUS CHRIST WAS NOT SENT TO ALL NATIONS

(Swahili Language)